24 Novemba 2014 - 19:29
Livni apinga sheria za kibaguzi za Israel

Pingamizi hilo la Livni linakuja huku akisisitiza yeye na wanasiasa wenzake wenye misimamo ya wastani serikalini hawataruhusu kupitishwa kwa sheria inayotamka kuwa Israel ni taifa lenye asili ya wananchi wa Kiyahudi pekee

Waziri wa Sheria wa Israel, Tzipi Livni, amesema leo iwapo Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, atalazimisha mswada tete kuhusu hadhi maalumu kwa Wayahudi kuwa sheria kupitia kura bungeni, huenda ikamaanisha kuwa kikomo cha serikali yake na kuitishwa kwa uchaguzi wa mapema nchini humo.

Pingamizi hilo la Livni linakuja huku akisisitiza yeye na wanasiasa wenzake wenye misimamo ya wastani serikalini hawataruhusu kupitishwa kwa sheria inayotamka kuwa Israel ni taifa lenye asili ya wananchi wa Kiyahudi pekee na kwani hiyo inakwenda kinyume na taswira yake ya kidemokrasia. Netanyahu amesema kwa mswada huo, Israel itakuwa haitambuliki tena kuambatana na sheria za kimsingi kama ni taifa la Kiyahudi na la kidemokrasia, bali ni makaazi ya kitaifa ya wananchi wa Kiyahudi litaleta usawa, lakini wanaoupinga wanasema itawabagua Waisrael wenye asili ya Kiarabu.

 

Lebo